HOSPITALI YA AGA KHAN YABORESHWA ZAIDI KWA KUONGEZA TAWI JIPYA KATIKA WILAYA YA KIGAMBONI.



Katibu tawala wa wilaya ya Kigamboni Rahel Muhando akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua huduma katika hospital hiyo mapema siku ya leo.


Katibu tawala wa wilaya ya Kigamboni akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa Kituo hicho cha huduma Katika wilaya ya Kigamboni huku akimuwakilisha Naibu waziri wa Afya jamii wazee na watoto.


Baadhi ya Mashine zinazopatikana katika Hospital hiyo ya Aga khan tawi la kigamboni.


Mgeni Rasmi akiwa kwenye Picha ya Pamoja na watendaji wa Hospitali hiyo.

Taarifa na Gasper Pascal

Taasisi ya huduma za afya Aga khana tawi la kigamboni jijini Dar es Salaam yatakiwa kutoa huduma ya matibabu kwa bei nafuu kwa lengo la kuwarahisishia wananchi wa kipato cha chini kupata huduma hospitalini hapo.

Hayo yamesemwa leo na Katibu wa Wilaya ya kigamboni Rachael Muhando wakati wa uzinduzi wa Hospitai ya Aga Khan tawi LA kigamboni na kutoa rai kwa taasisi hiyo kutoa huduma za matibabu kwa bei nafuu ili waweze kuwapa fursa wakazi wa maeneo hayo kupata huduma za afya kutoka katika hosptali hiyo.

" Kufunguliwa kwa kituo hiki ni fursa nzuri kwa wananchi wote hasa wakazi wa kigamboni kupata huduma iliyo bora"Amesema Muhando.

Amesema kuwa ni faraja na furaha kuona upanuaji wa huduma za afya kwa kuongeza hospitali karibu zaidi zinazotolewa na kusaidia kupunguza, kuondoa kwa kiasi kikubwa wagonjwa wanaokwenda kutafuta huduma nje ya nchi.

Aidha ametoa wito kwa watoa huduma wote wa Taasisi hiyo kutumia lugha ya kitabibu wakati wanapohudumia wagonjwa wao kwani kwa kufanya hivyo kutachangia kuongeza faraja na afueni kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo.

Bi Muhando amewataka watanzania kuchukua taadhari ya Ugonjwa wa UKIMWI kwani kinga ni bora kuliko tiba na kuwaasa wananchi kutowatenga na kutokuwanyanyapaa wenye Ugonjwa huo ukuzingatia leo ni Siku ya Maadhimisho ya Ugonjwa wa Ukimwi duniani kote.

"Leo ikiwa ni siku ya UKIMWI duniani Kila mwananchi anapaswa kuchukua tahadhari hasa ukizingatia Ugonjwa huu hauna tiba hivyo kinga ni bora zaidi" amesema Bi.Muhando



Kwa upande wake Mkurugenzi Uendeshaji wa vituo Afya Aga Khan Tanzania Bw. Fayaz Mohamed amesema huduma zitakazotolewa ni zile zile zinazotolewa katika hospital ya Aga khan na kuwataka wananchi kuacha kufikiri kuwa hopitali hiyo ni ya matajiri tu, amewatoa hofu kwani mtu yeyote mwenye kipato cha chini na cha juu wanaweza kutibiwa hapo.

Ameongeza kuwa watahakikisha tawi hilo la hospitali ya Aga Khan kigamboni wanajiunga na Bima ya Afya NHIF ili kurahisisha matibabu kwa wananchi na wakazi wa maeneo ya karibu.
  
Naye  Mkurugenzi wa Uuguzi Taasisi za huduma za Afya Aga Khan Tanzania Mama Lucy Hwai amesema wamefungua kitengo maeneo ya kigamboni ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma kwa urahisi zaidi, na kusema huduma zitakazotolewa ni za Mama na mtoto pamoja na matibabu mbalimbali.

"Niwaombe wananchi na wakazi wa maeneo haya kuweza kutumia huduma hii kwani imerahisishwa kwa kuletwa karibu kabisa ili kila mtu aweze kupata kwa urahisi kabisa" Amesema Lucy Hwai.