MBURAHATI WAZAZI SACCOS YAPATA USAJILI , MAPUNDA ASEMA SASA KAZI IMEANZA,CHET KATIBA ,VYOTE VIKO MKONONI

Mwenyekiti wa Wazazi Mburahati SCCOS (Ltd )ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Mburahati, John Mapunda aliye upande wa kushoto akiwa na baadhi ya viongozi .

Mwenyekiti wa Wazazi Mburahati Saccos Ltd ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Mburahati, John Mapunda amesema wanachama 100 wameshajisajili huku akibainisha kuwa Disemba 16 mwaka huu Saccos hiyo itazinduliwa rasmi katika Ukumbi wa Mburahati jijini Dar es Salaam.

Kauli hiyo ameitoa jijiini humo wakati wa upigaji kura za kumchangua Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Mkoa wa Dar es Salaam, wawakilishi na wajumbe wa jumuiya hiyo.

Amesema tayari Saccos hiyo imefanikiwa kupata usajili na kwamba siku hiyo itatumika kuongeza wananchama na kufanya harambee kwa viongozi na wadau watakaohudhuria.

" Tunatarajia kumpata mgeni rasmi hasa mkuu wa mkoa tunaamini watasaidia kufanikisha harambee itakayoendeshwa na wanachama kujiunga kwa wingi," amesema.


Amebainisha kuwa watu 500 wanatarajiwa kuhudhuria uzinduzi huo na kuwaomba wananchi kujitokeza kuchangamkia fursa ya kuwa wanachama wa Saccos hiyo.


Cheti cha usajili wa Wazazi Mburahati SACCOS Ltd


Katiba ya SACCOS ya Wazazi Mburahati SACCOS Ltd