DK. SHIKA NA MPYA TAREHE 9 DECEMBER.

 Meneja wa Dk Shika Catherine Kahabi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

Bilionea Dk Shika (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo na kuwataka wakazi wa Dar es Salaam kufika katika hafla hiyo.


Dk.Luis Shika  ni miongoni mwa watu waliopata umaarufu  mkubwa kwa muda mfupi kutokana na kushinda mnada wa nyumba za Tajiri Lugumi n kuweza kumweka katika muonekano wa ubilionea.

Dk  Shika anatarajia kukonga nyoyo za wakazi wa Dar es salaam siku ya tarehe 9 Desemba mwaka huu, katika hafla ya usiku wa 900 Itapendeza itakayofanyika ukumbi wa Dar live Mbagala ambapo ataongea na kuelezea historia yake alipotoka na alipo kwa sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari Leo Meneja wa Bilionea Dk Shika   Catherine Kahabi, amesema  hafla hiyo iliyopewa jina ya Usiku wa 900 Itapendeza lengo likiwa ni kumtambulisha Dk Luis Shika kwa wakazi wa Dar es Salaam , waweze kumfahamu zaidi.

Amesema katika hafla hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali wakiwemo wasanii wachekeshaji, akiwemo Mc pilipili, wasanii wa bongo fleva pamoja na bendi mbalimbali zitatumbuiza.

Aidha Mgeni rasmi.katika hafla hiyo anatarajiwa kuwa aliyekuwa waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi Lawrence Masha.