MUDA WA KUTOA MATIBABU BURE NDANI YA MELI YA KICHINA UMEONGEZWA .
Kutokana na Idadi kubwa ya Wananchi waliojitokeza kwenye *Zoezi Upimaji na Matibabu Bure* ndani ya *Meli ya Jeshi la Jamuhuri ya China*, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. PAUL MAKONDA* ameongeza nguvu kazi ya *Madaktari Bingwa* kwaajili ya kuhakikisha *kila aliepatiwa namba anahudumiwa*
Katika kikao Kati ya *RC MAKONDA* na Kamanda wa Jeshi la Jamuhuri ya China, *Madaktari wa China wameridhia kuongeza muda wa kutoa huduma* kwa *kupunguza muda wa Mapumziko* kutoka masaa Matatu hadi lisaa limoja pamoja na *kutoa matibabu usiku na Mchana.*
Aidha *RC MAKONDA* amesema kuwa *wameongeza Vituo Vitatu vya kutolea huduma* ambapo wapo watakaotibiwa eneo linalotumika kugawa namba *(central), pembezoni mwa Meli na ndani ya Meli kwa wale wagonjwa weliozidiwa Sana*.
Aidha *RC MAKONDA* amesema hadi sasa zaidi ya *Wagonjwa 17 wamefanyiwa Upasuaji Mkubwa Bure* kitendo ambacho kimesaidia kupunguza gharama za matibabu ikiwemo kusafirisha wagonjwa Nje ya Nchi.
Post a Comment