UJURUMANI YAFANYA MAZUNGUMZO NA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MHE:PAUL MAKONDA.

Balozi wa Ujerumani  Amb.Detlef Waechte akutana na kufanya mazungumzo na  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda  kuhusu changamoto zinazokabili mkoa huu.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Mh Makonda amesema  Balozi huyo amtembelea Tanzania na kumtaka aeleze changamoto zinazowakabili,  na kuhaidi kuzitekeleza kadri awezavyo.

Aidha amesema amemueleza balozi huyo changamoto katika sekta ya Afya,katika sekta ya elimu ambapo kuna ujenzi wa ofisi za walimu, pamoja na  kupambana na madawa ya kulevya, ambapo ameahidi kushirikiana kikamilifu katika kupunguza na kuondo kabisa tatizo hilo.

Pia amemshukuru  sambamba na kufurahishwa na balozi huyo kuja kwake,na kuweza kumtembelea, na kuweza kuangalia changamoto zinazooabili mkoa huu kikamilifu.