Serikali imepiga marufuku utoaji wa fedha
Serikali imepiga marufuku utoaji wa fedha kwa wakandarasi ambao hawajaonyesha tafiti za uhalisia wa eneo wanalokwenda kufanyia kazi ili kuepuka gharama na hasara na ziada ya fedha zinazoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi husika.
Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mheshimiwa Juma Aweso mara baada ya kukutana na viongozi, wafanyakazi pamoja na wanafunzi wa chuo cha maji nakusema serikali imejiwekea mipango mikubwa ya kumaliza tatizo la maji ikiwa ni pamoja na kusimamia wataalamu wake wanafanya kazi kwa uweledi na kutatua tatizo la maji ambalo limekua sugu kwa miaka mingi.
Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho Dkt.Shija Kazumba ameiomba serikali kuboresha miundombinu wanayoitumia ili kuendana na kasi ya dunia
Post a Comment