MOI yafanya upasuaji wa ubongo uliokuwa nje

Taasisi ya Mifupa (MOI) imefanikisha kufanya upasuaji mkubwa wa kurudisha ubongo wa mtoto wa miezi minne ndani ya kichwa baada ya mtoto huyo kuzaliwa huku ubongo wake ukiwa kwenye mfuko nje ya kichwa
Upasuaji huo wa kipekee umefanywa kwa zaidi ya saa manne na jopo la Madaktari bingwa wa ubongo na mgongo, wakiongozwa na Dkt Nicephorus Rutabasibwa ambao wote kwa pamoja ndani ya kipindi cha miezi miwili walikuwa wakitafiti namna bora ya kumfanyia upasuaji mtoto huyo.
Aidha kutokana na tafiti hizo ilionekana kwamba mtoto huto alizaliwa na uvimbe ambao ulikuwa umefunika sehemu kubwa ya ubongo na mishipa ya damu hali ambayo ingehatarisha maisha na ukuaji wake kwa ujumla.
Kwa mijibu wa taarifa iliyotolewa na taasisi ya Moi iesema kwamba Madaktari hao wamekumbwa na changamoto kadha wa kdha wakati wanatekeleza jukumu hilo la upasuaji ikiwa ni pamoja na mishipa midogo sana ya mtoto huyo ambayo imepelekea asiliia kubwa ya ubongo wa mtoto huyo kuwa kwenye uvimbe hali iliyowafanya madaktari kutafuta namna ya kuurudisha ubongo huo sehemu husika.
Imeaminika kuwa upasuaji huo wa kipekee umefanikiwa baada ya kuwepo na vifaa vya kisasa kwenye chumba cha upasuaji MOI pamoja na umahiri na uzalendo wa madaktari