Zitto Kabwe aibua mazito
Mbunge wa Kigoma Mjini ambaye hapo jana alikamatwa na jeshi la polisi jijini Dar es salaam, amekemea kitendo cha jeshi hilo kukamata watu ikiwemo Meya wa jiji la Mwanza, aliyekamatwa wakati wa msafara wa Rais Magufuli alipowasili mkoani humo, pamoja
Kwenye ukurasa wake wa facebook Zitto Kabwe ameandika ujumbe akisema kuwa hata hivyo Meya wa Mwanza James Bwire ana bahati ya kuachiwa siku hiyo hiyo, kwani mwenzake wa Manispaa ya Kibondo Simon Kanguye alikamatwa na hajaonekana mpaka leo.
"Juzi Meya wa Jiji la Mwanza ndg. James Bwire alikamatwa na kuwekwa ndani wakati wa ziara ya Rais huko Mwanza. Ninalaani tabia ambayo imeanza kushika mizizi ya kukamata viongozi wa serikali za mitaa nyakati za ziara za viongozi wakuu. Meya Bwire ana bahati, mwenzake wa Kibondo ndugu Simon Kanguye alikamatwa siku moja kabla ya Rais kufika Kigoma tarehe 21 Julai 2017 na hajaonekana mpaka Leo", ameandika Zitto Kabwe.
Kutokana na hilo Zitto Kabwe ameutaka uongozi wa Serikali za Mitaa Taifa (ALAT) kukemea vitendo hivyo vya unyanyasaji wa watumishi wake.
Soma hapa chini
Post a Comment