Kiongozi Mkuu Chadema avunja ukimya

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr. Vicent Mashinji‏ ametupa jiwe gizani na kudai kwamba kitendo cha dola kumkamata mtu kwa tuhuma za uchochezi ni udhaifu wa serikali katika kujibu hoja.
Dr. Mashinji amesema kwamba siasa zenye msamiati wa  uchochezi huwa hazipo hivyo kwani wadhaifu huwa ndiyo wanaotumia mabavu na siyo hoja.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Dkt Mashinji ameandika "Najenga hoja, unasema mi mchochezi. Kweli umekosa ushawishi jitafakari upya, siasa za sasa msamiati wa uchochezi haupo. Ni hoja kwa hoja!"
Hivi karibuni viongozi mbalimbali wa upinzani wamekuwa wakikamatwa na jeshi la polisi mara kwa mara kwa tuhuma za uchochezi.