Bodi yaufunga uwanja wa mpira

Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi TPLB, Boniface Wambura amesema wanaendelea kuboresha ligi kuu ya soka Tanzania bara kwa kushughulikia mapungufu mbalimbali ikiwemo viwanja.
Akiongea na wanahabari leo Wambura amesema wameufungia uwanja wa Jamhuri Morogoro usitumike kwenye michezo ya Ligi kuu kutokana na kuwa na mapungufu mbalimbali ambayo yanahitaji kufanyiwa marekebisho.
“Tunahitaji kuboresha zaidi ligi yetu na tunazifanyia kazi changamoto ambazo zinajitokeza, hivyo tunaomba wadau wawasilishe malalamiko yenye ushahidi kwani yatapokelewa na kufanyiwa kazi”, amesema Wambura
Aidha Wambura amewaasa viongozi wa timu zinazoshiriki ligi kuu kuishirikisha bodi pale wanapohisi kuna mapungufu ili iweze kuboresha. Sambamba na hilo Wambura amesema wanaendelea kuongeza umakini kwa waamuzi ili kuondoa kasoro ndogondogo kwenye maamuzi.