Tutauza Figo zetu - Lema
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amewajulisha wananchi wa Singida Mashariki (jimboni kwa Lissu) kwamba kupigania kwao uhai wa Mbunge Tundu Lissu hakutakoma kwani hakuna thamani yenye kufikia thamani ya kiongozi huyo.
Lema ameyasema hayo kwenye kampeni za uchaguzi mdogo Kata ya Siuyu ambapo amefafanua kwamba japokuwa serikali na bunge havikuweza kushughulikia matibabu ya Mbunge huyo wao wataendelea kupambana.
"Matibabu ya Lissu mpaka sasa ni takribani Milioni 500 zimetumika. Serikali imekataa kulipa, bunge limekataa lakini nyie mmechanga thumni thumni zinaendelea kumponya na hata kama zitafika trilion tutauza hata figo zetu kwa ajili yake ili apate uponaji" Lema.
Lissu alipigwa risasi Septemba 7 mwaka huu na watu wasiojulikana akiwa Mkoni Dodoma na kisha kupelekwa Nairobi kwa ajili ya matibabu.
Post a Comment