Mugabe atimuliwa rasmi

Kamati Kuu ya Chama Tawala cha Zanu - Pf, nchini Zimbabwe, imemfuta rasmi Uenyekiti wa chama hicho Rais Robert Mugabe
Aidha, kamati hiyo imemteua aliyekuwa Makamu wa Rais, Emmerson Mnagangwa kuongoza chama hicho na kumtaka Mugabe ajiuzulu mwenyewe Urais au ang'olewa madarakani kwa lazima kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na bunge la nchi hiyo.
Kadhalika chama hicho kimemfutia uanachama mke wa Rais Mugabe, Grace Mugabe, hatua hiyo inamnyang'anya moja kwa moja cheo cha Uenyekiti wa Baraza la Wanawake la chama hicho.
Rais Mugabe anatarajiwa kukutana na viongozi wa kijeshi baadaye leo ambapo msafara wake ulionekana ukiondoka katika makazi yake binafsi jijini Harare ambako amekuwa katika kizuizi cha nyumbani.
Jana Jumamosi maelfu ya raia wa Zimbabwe walindamana katika mitaa ya jiji la Harare kumpinga Rais Mugabe.