Barnaba ashindwa kujizuia kwa Mama Steve
Mwanamuziki anayefanya poa kwenye game ya Bongofleva Barnaba Classic ameshindwa kujizuia kwenye siku ya kuzaliwa mama wa mtoto wake Zuwena ambaye kwa sasa hawapo pamoja kwa kumshukuru kuwepo na kumpatia zawadi ya mtoto.
Barnaba akiwa na aliyekuwa mpenzi wake Zuu |
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Barnaba amesema kwamba upendo wake juu ya zawadi mwanadada huyo aliyempati ipo palepale na kusisitiza kwamba anamuheshimu huku akimsisitizia kwamba anapenda kumuona akiwa furaha.
"Wewe ni rafiki Yangu na ndugu yangu Uvungu wa moyo wangu unakushukuru kwa kuwa daraja kwenye maisha yangu na nashukuru nimevuka salama matatizo ni sehemu ya kila mwanadamu upendo wangu juu ya zawadi uliyonipatia Iko pale pale/STEVE Na Kitu kizuri ninakuheshimu Sana mbali Na mambo Yote Na Kitu kingine Furaha Yangu kuona unaendela Kutabasamu Hata kama ilo Tabasamu Silitengenezi Mimi," Barnaba
Aidha Barnaba ameongeza kwamba anamtakia kila la kheri mwanadada huyo ambaye tayari amekwishaingia kwenye mahusiano na kumwambia anapenda yeye awe shuhuda wa maisha ya mzazi mwenzake huyo kwa kila jambo.
"Nakutakia maisha mema yenye baraka, nawaombea heri Katika Familia yako, nakuombea heri na uwahi uwe shuhuda wangu nami niwe shuhuda wako wa kila jambo heri ya siku yako ya kuzaliwa mzazi mwenzangu mama yake Steve, Zuunamela mama watoto ! Damu Ya yesu ikuangazie Amina," Barnaba
Post a Comment