Simba yatoa kipigo
Klabu ya soka ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Rukwa Stars uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga.
Katika mchezo huo Rukwa Stars ndio ilikuwa ya kwanza kufunga bao la kuonngoza, lililofungwa dakika ya 19 kupitia kwa Adam Matogwa. Baadae dakika ya 21 Simba ikasawazisha kupitia kwa Mohamed Ibrahim na kufanya kipindi cha kwanza kimalizike kwa 1-1.
Kipindi cha pili Simba ilifanikiwa kuandika bao la pili dakika ya 47 kupitia kwa mshambuliaji Juma Luizio. Sekunde kadhaa kabla ya mpira kumalizika Simba ilifanikiwa kufunga bao la tatu kupitia kwa Juma Luizio ambaye amefunga mabao mawili katika mcheo huo.
Simba inaendelea na michezo ya kirafiki kwenye mikoa ya kusini ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wake wa ligi kuu utakaopigwa Novemba 19 jijini Mbeya dhidi ya Tanzania Prisons.
Post a Comment