Serikali yazungumzia majeruhi wa bomu Kagera

Serikali ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera, imesema majeruhi 11 wa bomu waliolazwa hospitali ya Rulenge wilayani humo wataendelea kuwepo chini ya uangalizi wa madaktari bingwa waliotoka Hospitali ya Rufaa Bugando iliyopo Jijini Mwanza
Hayo yamesemwa na na kuwekwa wazi na Mkuu wa wilaya ya Ngara Luteni Michael Mtenjele leo hii wakati akiongea na waandishi wa habari na kusema kwamba hali za majeruhi hao zinaonesha matumaini kiafya kutokana na juhudi za wataalamu wa afya
Aidha ameweka wazi kwamba wagonjwa hao wanaendelea kuhudumiwa na waganga kwa kuwahudumia majeraha baada ya kufanyiwa nao upasuaji na hofu kubwa ilikuwa ni upungufu wa damu lakini wananchi wengi wamejitokeza kutoa damu kwa majeruhi hao.
“Tumepata msaada mwingine kutoka benki ya damu ya wilaya jirani ya Karagwe vikiwemo vifa tiba na dawa kutoka zahanati za jirani, MSD tawi la Muleba na Ofisi ya mganga mkuu wa mkoa.” Amesema Kanali Mtenjele.
Novemba 8 katika Shule ya msingi Kihinga ulitokea mlipuko wa bomu uliosababisha vifo vya wanafunzi pamoja na jerhi baada ya mwanafunzi mmoja kufika na bomu hilo shuleni hapo akidhani kwamba ni chuma.