RC MAKONDA AONGEZA MUDA WA TAMASHA LA FIESTA KWA MASHARTI
Kufuatia Mazungumzo Marefu ya Kina baina ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. PAUL MAKONDA na Uongozi wa Clouds Media ameridhia kuongeza Masaa Machache ya Tamasha la Fiesta kwenye Viwanja vya Leaders Club ili kuruhusu Wasanii Wote kutumbuiza.
Katika Mazungumzo hayo RC MAKONDA aliwataka Clouds kuchagua Kati ya kufanya Tamasha hilo kwenye Uwanja wa Uhuru ili wapige Mziki hadi Asubuhi au kufanya kwenye Viwanja vya Leaders Club Clouds ambapo Clouds walichagua kufanya Tamasha hilo Viwanja vya Leaders Club na wapo tayari kufuata Sharti la kutoongeza Muda waliokubaliana.
Aidha RC MAKONDA amesema kuwa baada ya Tamasha Hatoruhusu tena Viwanja vya Leaders Club kutumika kwa Matamasha ya Usiku kwakuwa ni Usumbufu wa Wakazi na Ofisi za Bilozi zilizopo jirani na Viwanja hivyo.
Amesema kuwa Viwanja hivyo kwa sasa vitatumika kwa Matukio ya Nyakati za Mchana pekee hivyo kwa anaetaka kufanya Tamasha la kukesha atumie Uwanja wa Uhuru ambao umefunikwa na haupo karibu na Makazi ya Watu.
Amewataka Wananchi kufuata Sheria, Kanuni na taratibu zilizowekwa na Serikali na kusisitiza kuwa Sheria haina upendeleo kwa yoyote.
Amewasihi Wadau wa maendeleo kuwekeza katika Ujenzi wa Kumbi kubwa zenye Soundproof na uwezo wa kubeba watu Wengi ili zitumike kwenye matamasha ya kukesha.
Post a Comment