HATIMAE MELI YA JAMUHURI YA CHINA YENYE HOSPITALI NDANI KUONDOA NANGA,
TAARIFA NA GASPER PASCAL
Zoezi la upimaji afya kwa wananchini wa Mkoa wa Dar es salaam , lililo fanywa na madaktari kutoka china na kufanyika ndani ya Meli ya kijeshi ya Jamuhuri ya China , leo limefungwa rasmi katika Bandari ya Dar es salaam.
Akizungumza katika tafrija ya kuwaaga madaktari walioshiriki katika zoezi hilo Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amemshukuru balozi wa China Jeshi, na Madaktari waliofika kuwahudumia wananchi na kueleza dhamira ya serikali ya ya awamu ya tano kuwa ni kugusa moja kwa moja wananchi kwa kutatua changamoto ikiwemo kuboresha huduma za Afya ..
Amesema niupendo wa pekee kwa nchi ya china kwa watanzania kwa kuwa wamewahudumia watanzania kwa upendo kwa kuwapatia chakula , malazi na matibabu, hii ni kwa sababu ya mahusiano mazuri aliyo yafanya hayati Baba wa Taifa mwalimu JK Nyerere .
Kwa upande wake Mganga mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Grace Magembe akitoa taarifa ya jumla ya kazi iliyofanywa na madactari hao amesema wananchi walijitokeza kwa wingi zaidi ya Idadi iliyo tarajiwa ya watu 3000 na wakajitokeza zaid ya elf kumi ambapo wametibiwa wagonjwa 2463 ndani ya Meli na wagonjwa 561 wa walitibiwa kwa nje ya meli katika hospitali za wilaya za mkoa wa Dar es salaam na kusema kuwa wagojwa 23 walifanyiwa upasuaji ndani ya meli na 88 walihudumiwa na Madaktari wa MOI na JKCI.
Naye kiongozi wa Meli hiyo Amemshukuru Makonda kwa kuwa kunabaadhi ya mambo kuna wakati yalipokuwa yanataka kukwama alisaidia na kazi zikaendelea kama kawaida,na kueleza kuwa Meli hiyo yenye hospitali ilishawahi kuja tanzania miaka saba iliyo pita na kwamba ninadra sana kupata nafasi ya kutembelewa na meli hiyo ila Tanzani ni moja ya nchi ambazo sasa Meli hiyo imetembelea mara mbili.
`Pia katika hafla hiyo ya kuwaaga madaktari wa China ,Watanzania pamoja na Wachina wamepata nafsi ya kula,kunywa na kucheza tamaduni zao kwa pamoja na kuonyeshana michezo mbali mbali kutoka kila nchi.
Post a Comment