RC MAKONDA AWATOA HOFU WAGONJWA WOTE.
TAARIFA NA GASPER PASCAL
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe:Paul Makonda,amewatembelea wagonjwa waliojitokeza kupewa matibabu ya bure katika meli ya Jamhuri ya China iliyotia nanga mnamo tarehe 19 /11 /2017 katika bandari ya Dar es salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe:Paul Makonda,amewatembelea wagonjwa waliojitokeza kupewa matibabu ya bure katika meli ya Jamhuri ya China iliyotia nanga mnamo tarehe 19 /11 /2017 katika bandari ya Dar es salaam.
Mkuu wa mkoa amewatoa hofu wagonjwa wote wenye uhitaji wa huduma ya matibabu bure na kusema kuwa wote waliojitokeza watapewa matibabu vile inavyotakiwa na kuwataka wagonjwa hao waendelee kuwa na imani na madaktari wao ili wachina watakapoondoka nchini waendelee kutibiwa kama kawaida kwa wale watakao kuwa bado huduma hii haijawafikia,kwani wachina waliahidi kuhudumia wagonjwa kwa muda wa siku saba tu.
Pia amewataka wagonjwa wale wenye uwezo wa kipato waendelee kujihudumia katika hospital za taifa na huduma hii ya matibabu bure waiache kuwa kipaumbele kwa wanyonge wasiojiweza katika swala la kipato.Rc Makonda ameyasema hayo wakati akiwa katika kituo cha kutolea huduma ndogo ya matibabu bure
Vilele Mhe:Paul makonda alipata nafasi ya kuwatembelea wagonjwa waliokuwa tayari wamefanikiwa kupatiwa huduma ya matibu bure katika meli ya kichina na kujionea jinsi ambavyo wagonjwa wa operesheni wanavyoendelea vizuri na afya zao kuonekana kuimarika zaidi.
Katika hatua hiyo,Wagonjwa walionekana kumshukuru Mhe:Makonda kwa kuwa ameweza kuwaletea matibabu bure ambayo kwa hali ya kawaida wangetakiwa kutibiwa kwa gharama za hali ya juu sana na hata wengine kutakiwa kwenda nje ya nchi.
Post a Comment