Nyalandu apongezwa

Baada ya kujitangaza kupitia vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii kuhusu kujiuzulu  nafasi zake za uongozi ikiwa na ya Ubunge, wananchi mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii wamempongeza  Nyalandu kuhusiana na maamuzi hayo huku wakimtaja
kiongozi huyo kama shujaa kwa maamuzi aliyofanya. 
Kupitia katika ujumbe huo wa kujiuzulu uliowekwa na kiongozi huyo wananchi wengi wamemsifu kwamba ameauchagua  upande wa haki. 
Hata hivyo baadhi ya maoni wananchi wamemuandikia Nyalandu kwamba ameilinda na kuitunza Katiba kwa kuwa mkweli kwa wanaokwenda kinyume na katiba na pia wameahidi kwamba wanamuunga mkono.
Fuatilia hapa chini baadhi ya maoni ya wananchi kwenye ukurasa wa Mbunge Nyalandu