Mdee amtahadharisha Nyalandu kuhusu CHADEMA
Mbunge wa Kawe jijini Dar es salaam Halima Mdee amemkaribisha aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini ndani ya chama chao huku akimtahadharisha kuhusu changamoto wanazokumbana nazo viongozi wa chama hicho.
Halima Mdee ametumia mtandao wake wa kijamii wa Twitter kumkaribisha Nyalandu ambaye leo ametangaza kujiuzulu nafasi zake za uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi pamoja na nafasi yake ya ubunge aliokuwa nao.
"Mhe. Nyalandu karibu sana CHADEMA. Naamini utakuwa imara kukabiliana na siasa za chuki, ubaguzi na visasi zinazolikabili taifa letu".
Mapema leo Mh. Nyalandu ambaye alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM litangaza kujiuzulu nafasi zake hizo kwa kile alichodai kwamba hafurahishwa na mambo ya kisiasa yanayoendelea nchini na kuwaomba wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kama wataridhia wampe nafasi ili kuweza kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi kupitia chama hicho.
Post a Comment