Gib Carter ajivunia 'Wizkid'

Msanii wa muziki wa bongo fleva 'Gib Carter' ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Sawala' amefunguka na kusema anajivunia watu kumfananisha na mkali kutoka Nigeria Star Boy na kusema hiyo inaonyesha kuwa uwezo wake kimuziki ni wa juu.
Akipiga stori na EATV Gib Carter amedai kuwa anafurahi kuona anatoka kimuziki na kuanza kufafanisha na msanii mkubwa barani Afrika na ulimwenguni  Wizkid na kusema hiyo ni dalili njema kuwa yeye ni star kwa bongo na hali hiyo inaelezea ukubwa wa kipaji chake.