Mvua zinazoendelea Dar: Mmoja aripotiwa kufariki, ripoti kamili iko hapa

Mtu mmoja anaripotiwa kufariki dunia kutokana na mvua zinazo endelea jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Kamanda Mkoa wa kipolisi Ilala Salum Hamduni ameeleza kuwa mvua zinazo endelea jijini Dar es Salaam zimeweza kupoteza maisha ya kijana Mmoja maeneo ya Tabata Kimanga, Mto Kenge ambaye anakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 mpaka 30.
RPC Hamduni ameeleza kuwa taarifa za kijana huyo kuhusu majina yake bado hazija kamilika, na kuhusu uharibifu wa mali amehaidi kutoa ufafanuzi hapo baadae.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akimuonesha Mbunge wa jimbo la Ilala Mussa Hassan Zungu baadhi ya nyumba zilizoharibiwa na mvua (nyumba hazipo pichani)Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewataka wakazi wote wanaosihi maeneo hatarishi hususani Jangwani kuondoka mara moja kwani mvua hizi ni endelevu na huenda zikafika mpaka siku ya Jumamosi hivyo ni vyema kuchukua tahadhari kwa kuhama maeneo na kwenda maeneo yaliyo salama.
Barabara kuelekea Jangwani ikiwa imefungwa