RC Makonda: Dar es Salaam kuwa sehemu pekee ya kuuzia magari barani Afrika
Mkuu wa mkoa Dar es salam Paul Makonda ameeleza kuwa ndoto yake kubwa nikuifanya Dar es salaam kuwa sehemu pekee ya kuuzia magari katika bara la Afrika, kwahiyo kukamilika kwake, kutaongezea pato la taifa
Ameyasema hayo akiwa ameambatana na maofisa kadhaa wa serikali na wa jeshi la polisi walipotembelea eneo maalumu la kuuzia na kununua magari katika eneo la Kigamboni kwa lengo la kuona maendeleo ya miundo mbinu, sambamba na kutazama walioomba kama wameshaamza kujenga, maendeleo ya ujenzi wa Barabara, ambapo aliongeza kuwa amefarijika baada ya kukuta tayari baadhi ya wawekezaji wameshaanza ujenzi wa maeneo yao
Edwin chande meneja wa mabohari ya fordha, ameeleza kuwa wao kama mamlaka ya mapato wanaona kama kukamilika kwa mradi huo itakuwa ni chachu ya ongezeko la kodi na pato la taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Xavier Lukuvi meneja wa mipango na uwezeshaji NSSF, ametangaza kwa kuwatoa hofu Wajasiriamali na wote wenye nia ya kufanya biashara ya uuzaji magari kuwa watawawezesha wananchi kwa vikundi au mmoja mmoja kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu na hivyo wasisite kujitokeza.
Baada ya kukabidhiwa eneo la kiusalama lenye mita za mraba elfu 30, SACP Lazaro Mambosasa amewahakikishia ulinzi na usalama wawekezaji wote sambamba na kuomba jeshi la polisi ndio liwe la kwanza kuanza ili kuwapokea na kuwalinda wawekezaji.
Geofrey Silanda meneja usalama barabarani na mazingira nchini kutoka mamlaka ya usafiri wa majini na nchi kavu ameeleza kuwa kukamilika kwa mpango huo itarahisisha kuyadhibiti kwa uharaka magari mengi na kwa pamoja.
Kwa uapande wake Mkurugenzi wa Property International bwana Halim Zaharan ambao ndio wamiliki wa eneo hilo amsema bado maeneo yapo na kwamba wawekezaji waendelee kujitokeza kufanya maombi ya kupatiwa maeneo hayo.
Post a Comment