Watanzania wenzangu tupinge kubaguana - Nyalandu
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amefunguka na kusema kila Mtanzania anapaswa kupinga moja kwa moja kuhusu vitendo mbalimbali vya kubaguana kwa itikadi za siasa au jambo jingine lolote na kusema wanapaswa kuwa na ubinadamu.
Lazaro Nyalandu amesema hayo wakati akieleza juu ya yeye kusaidia watu mbalimbali kuwapeleka hospitali kwa ajili ya matibabu na kusema yeye anafanya hivyo kwa kuwa anaguswa na si kwamba anafanya hivyo kwa ajili ya siasa au kutafuta sifa.
"Haya ni sehemu tu ya jinsi mimi nilivyo hatufanyi haya mambo kwa ajili ya sifa za kibanadamu bali tunafanya haya mambo kwa sababu tunaguswa, tunafanya kwa sababu ya ubinadamu na kwa kuwa sifa, utukufu na heshima zote zinamuendea Mungu" alisema Nyalandu
Aidha Mbunge huyo alisema katika kuguswa na jambo lolote lile hapo huwa mtu haangalii hilo jambo limemkuta nani au limemkuta mtu wa itikadi gani bali hufanya kwa lengo la kusaidia.
"Ukitaka nchi iwe nchi ya majuhaa, iwe nchi ya watu wa ajabu pambana na tofauti zao zozote zile, kwa hiyo natumia nafasi hii kuwaambia Watanzania wenzangu tupinge vitendo vya aina yoyote vya kubaguana tuongeze ubinadamu lakini cha muhimu mwenzetu anapokuwa ameumia kama vile Tundu Lissu ni jambo lililowagusa watu wote wa imani zote, itikadi zote wakubwa kwa wadogo na vyama vyote vya kisiasa na zaidi huyo ni ndugu yangu, kama kaka yangu mkubwa kutoka kule Singida tutashirikiana kuhakikisha kwamba mema yanamtokea" alisema Nyalandu n
Mbunge Lazaro Nyalandu ndiye Mbunge pekee wa Chama Cha Mapinduzi aliyefunga safari na kwenda kumuona Mbunge Tundu Lissu jijini Nairobi na kuhangaikia kutaka kufanikisha safari yake kwenda nje ya nchi kwa matibabu zaidi lakini mpango huo ulisimama kwanza kutokana na madaktari wa Nairobi kusema kwa sasa Mbunge huyo asingeweza kusafiri mpaka pale hali yake itakapotengemaa.
Post a Comment