Bashe ampinga msemaji wa serikali

Mbunge Hussein Bashe amefunguka na kumpinga Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas kuhusu kauli yake aliyotoa kwenye mtandao wake wa Twitter kuhusu mitandao ya kijamii kuchangia kuhatarisha usalama wa nchi na kusema kauli hiyo inatumika vibaya. 

Hussein Bashe alitumia mtandao wake wa Twitter pia kujibu hoja juu ya kauli ya Msemaji wa Serikali na kusema kuwa neno 'Usalama wa Nchi' muda mwingine linatumika vibaya kwa ajili ya kulinda utashi wa watu waliopo madarakani. 
"Usalama wa Nchi" muda mwingine neno hili hutumika vibaya kulinda Utashi wetu sisi watawala . Ni vizuri kuwapa watu nafasi ya kupumua" aliandika Hussein Bashe  
Jana baadhi ya viongozi wa serikali walikutana na wadau mbalimbali ambao walikuwa wakitoa maoni yao ili kuboresha kanuni za maudhui ya Utangazaji na Mitandao ya Kijamii ambapo Katibu Mkuu Wizara Habari Prof. Elisante ole Gabriel alisema kuwa mitandao ya kijamii inatoa habari kwa haraka na kusema mfumo wa sasa wa mitandao ya kijami unachangia kutoa taarifa za uongo, chuki na hata kuhatarisha usalama wa nchi.