"Sipo tayari kununua viewers"- Jay Moe
Mkongwe wa Hip hop Bongo, Jay Moe amefunguka na kudai hayupo tayari kununua watazamaji katika video zake kama wanavyofanya baadhi ya wasanii, kwa kuwa kufanya hivyo ni kujidanganya nafsi yako mwenyewe katika ufanyacho.
Mkongwe wa Hip hop Bongo, Jay Moe
Jay Moe ameeleza hayo baada ya kuwepo na uvumi wa muda mrefu ukidai kuna baadhi ya wasanii huwa wanatabia ya kununua 'viewers' katika kila kazi zao wanazoziweka katika mitandao ya kijamii ili kuwapumbaza wenzao kuwa video aliyoichia imevunja rekodi kwa kupendwa na watu.
"Sipo tayari kununua 'viewers' kama ningekuwa nataka kufanya hivyo ningefanya tokea katika video yangu ya nisaidie kushare kwa sababu nilifatwa na watu wakitaka kunifanyia hivyo na mpaka leo wananilaumu kwa kutowasikiliza mawazo yao, kwa maana huo wimbo hujaweza kufika hata Milioni 1 hadi sasa", amesema Jay Moe.
Pamoja na hayo Jay Moe ameendelea kwa kusema "Wananiambia kabisa 'we can do numbers' katika mazingira haya na haya, lakini mimi huwa nawambia wapo watu watakaopenda kufanya hivyo ila mimi mwenyewe inaweza isinigee 'actual number' zangu halali ni zipi?. Huwezi ukawa na hiyo demographic ukajua kwamba nakubariki na watu kiasi hichi kwa sababu ulidanganya hizo 'numbers"
Jay Moe kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya wa 'Me & You' ambao una wiki moja tokea auweke katika mtandao wake wa Youtube na kuweza kutazamwa na watu 65,541, Nisaidie Kushare ina miezi sita na kutazamwa jumla ya watu 400,961 huku Pesa ya madafu yenye mwaka mmoja ikiwa ndiyo video iliyotazamwa na wengi kwa kuweza kufikia 276,119.
Itazame hapa video mpya ya Jay Moe
Post a Comment