"Hatutawaacha mpaka nchi inyooke" - Mpango
Waziri wa fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema serikali haitaawacha kuwanyoosha watu wanaoendelea kuhujumu uchumi, kwa kuwachukulia hatua za kisheria, kwani wanaumiza Watanzania.
Waziri Mpango ameitoa kauli hiyo leo alipokuwa akipokea ripoti ya tathmini na utendaji wa taasisi za umma, iliyotolewa na bodi ya wakurugenzi (PPRA) na kusema kwamba serikali imejipanga kwa nguvu zote kupambana na vitendo vya rushwa hivyo watu hao lazima wawasilishwe TAKUKURU.
Waziri Mpango ameendelea kwa kusema kwamba katika taasisi 17 zilizobainika kufanya ubadhirifu wa fedha za umma ikiwemo zile anazozisimamia na miradi yote inayoendeshwa na kusema serikali itawawajibisha wote pasipo kuogopa mtu yeyote, kwani haiwezekani kuendelea kufuja mali za Watanzania kwa kiasi kikubwa.
"Hatuwezi kuendelea kutumia fedha za masikini namna hii, tutachukua hatua tutawawajibisha wote wanaohusika, hatuogopi mtu hapa, lazima tuhakikishe fedha za umma zinalindwa kwa nguvu zote, taarifa hii tutaifanyia kazi ipasavyo, na wote wanaohusika hatutaacha jiwe bila kuligeuza, tutalala nao mbele mpaka nchi ibadilike na inyooke", amesema Waziri Philip Mpango.
Miongoni mwa taasisi zilizotajwa kwenye ripoti hiyo kujihusisha na vitendo vya rushwa, ni pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ambayo ipo chini ya Wizara yake, na kuahidi kuanza kuishughulikia mwenyewe kabla ya mamlaka husika.
Post a Comment