MCT kukomesha udhalilishaji kwa wanahabari
Waziri wa fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema serikali haitaawacha kuwanyoosha watu wanaoendelea kuhujumu uchumi, kwa kuwachukulia hatua za kisheria, kwani wanaumiza Wata
Hayo yameelezwa na Ofisa Miradi wa Baraza hilo Bi. Pili Mtambalike katika Mkutano Mkuu wa MCT ambapo amesema matukio hayo yanaongeza hofu na kuwafanya waandishi washindwe kutimiza wajibu wao kikamilifu.
Bi. Mtambalike amesema kwa kipindi cha mwaka huu zaidi ya matukio 11 yameripotiwa na kusema kwamba wataanza kuwachukulia hatua ikiwamo kuwashtaki wale wote watakaofanya hivyo huku akiwaasa wanahabari kutoa taarifa vinapotokea vitendo vinavyokiuka uhuru wa habari.
Kwa upande wake rais wa MCT, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amesema baraza hilo lilianzisha Rejista ya Matukio ya Uvunjaji Haki wa Habari (PFVR) ili kuhakikisha kila tukio linaripotiwa na kuchukuliwa hatua lengo likiwa ni kuhakikisha kunakuwa na takwimu sahihi za matukio hayo ili wanapowasiliana na Serikali kuwe na mfano halisi.
Post a Comment