Serikali yakiri kuongezeka kwa vifo
Vifo vinavyotokana na uzazi vimeongezeka kutoka 432 kwa vizazi hadi laki moja katika kipindi cha mwaka 2012-2013 hadi kufikia 556 mwaka 2016-2017 sawa na kina mama 900 wanapoteza maisha kila mwezi na thelathini kila siku nchini wakati wa kujifungua.
Takwimu hizo zimetolewa jijini Dar es Salaam na waziri wa afya, Mhe. Ummy Mwalimu alipokuwa anapokea mashine ya kisasa ya kutoa dawa ya usingizi wakati wa upasuaji iliyotolewa na taasisi ya utepe mweupe ambapo amesema katika kukabiliana na tatizo hilo ifikapo mwezi juni 2018 serikali itaongeza vyumba vya upasuaji kutoka 109 hadi 279.
Akizungumza baada ya kukabidhi mashine hiyo mratibu wa kitaifa wa taasisi ya utepe mweupe Bi. Rose Mlay amesema ongezeko hilo la vifo linasikitisha na kumuomba waziri kuhakikisha anaendelea kuweka mkazo katika suala la upatikanaji wa huduma za dharura na kwa haraka kwa mama mjamzito hasa maeneo ya vijijini.
Kwa upande wake katibu mkuu wa wizara hiyo Dkt. Mpoki Ulisubisya ambaye pia ni mtaalamu wa usingizi ameelezea namna mashine hiyo inavyofanyakazi,uwezo wake na faida zake kwani haihitaji mitungi ya gesi wala umeme na ina uwezo wa kuonyesha viashiria vya hatari.
Post a Comment