Madawati yaziponza halmashauri saba
Bodi ya mfuko wa barabara nchini imeziagiza halmashauri saba zilizotumia fedha zaidi ya milioni 500 zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara nchini badala yake zikatumika kutengeneza madawati na maabara zirejeshe fedha hizo ndani ya mwezi mmoja.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini (RFB), Bw. Joseph Haule. |
Akitoa taarifa ya ukaguzi wa kiufundi na fedha kwa kazi za ujenzi Mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa barabara, Joseph Haule, ameziagiza halmashauri zilizofanya udanganyifu ambao ni kinyume na taratibu kuzirejesha fedha hizo katika mfuko wa barabara huku zaidi ya shilingi ya shilingi milioni 64 zikitumika katika miradi hewa.
Amesema Katika mwaka wa fedha 2015/16 bodi ya mfuko wa barabara nchini RFB kupitia wahandisi washauri ilifanya ukaguzi wa kiufundi wa miradi ya ujenzi na ukarabati wa barabara na madaraja ambapo jumla ya mikoa 22 na halmashauri zake zilikaguliwa
Kwa upande wake meneja wa bodi ya mfuko wa barabara, Eliud Nyauhenga, amesema bodi hiyo imetoa muda hadi Oktoba 30 mwaka huu kwa halmashauri zilizotumia fedha hizo zirejeshwe kwa ajili ya matumizi ya ujenzi wa barabara.
Miongoni mwa halmashauri zilizotajwa kukiuka matumizi ya fedha za mfuko wa barabara na kupeleka kwenye madawati na ujenzi wa maabara ni halmashauri ya wilaya ya Karagwe, Kyerwa, Ushetu, Masasi, Nanyumbu, Kilolo na halmashuri ya wilaya ya Songea.
Post a Comment