Kila mechi kwetu ni Fainali - Mbaraka Yusuph
Mshambuliaji tegemeo wa Azam FC, Mbaraka Yussuf amesema kila mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara kwao ni kama fainali.
Mshambuliaji tegemeo wa Azam FC, Mbaraka Yussuf |
Mbaraka Yussuf amesema wanajua ya kuwa kila mchezo wanaocheza unakuwa mgumu kutokana na timu pinzani kuwakamia, lakini amedai malengo yao ni kushinda kila mtanange.
“Kwanza namshukuru Mungu kucheza mechi hizi salama pia namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kufunga pia napenda sana kujitahidi kadiri ya uwezo wangu kila mechi niwe naweza kufunga ili niweze kuweka rekodi nzuri katika msimu huu na nawaahidi mashabiki kuwa mfungaji bora” amesema Mbaraka Yussuf
Akizungumzia kuhusu mchezo ujao dhidi ya Singida United, Mbaraka amesema:
“Kwa kweli mechi yoyote ile Azam ikikutana na timu yoyote mechi inakuwa ngumu kwa vile watu wanakuwa wanakamia sana, kauli mbiu yetu kila mechi sisi kwetu ni fainali na tunapambana ili tuweze kufunga. ” amesema.
Post a Comment