Rais Dkt. John Magufuli
Rais Dkt. John Magufuli amepokea ripoti ya uchunguzi wa madini ya Tanzanite na Almasi Ikulu jijini Dar Es Salaam.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa ripoti hizo Rais Magufuli ametaka watendaji waliotajwa kuhusika katika upotevu wa rasilimali za madini hayo kukaa pembeni.
Baada ya kukabidhiwa ripoti hizo Rais Magufuli amezikabidhi ripoti hizo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU ili zifanyiwe kazi.
Rais Magufuli amekabidhiwa ripoti hizo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya ripoti hizo kuwasilishwa kwa Spika wa bunge Job Ndugai aliyezikabidhi kwa Waziri Mkuu Majaliwa jana Jumatano Septemba sita mwaka 2017.
07 Septemba 2017
Post a Comment