Polisi waombwa kufanya uchunguzi wa kina utekwaji wa watoto Arusha

Responsive image
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo
Baadhi ya Wakazi wa kata ya Olasiti mkoani Arusha wameliomba jeshi la polisi mkoani humo kufanya uchunguzi wa kina kuhusu kutekwa kwa watoto pamoja na vifo vyao ili kubaini undani wa tukio hilo.
 Wakizungumza na TBC, Wazazi wa Watoto Maurine Njau na Iqramu Salimu wamesema wanajiandaa na taratibu za mazishi ya watoto wao lakini wanaomba uchunguzi wa kina ufanyike kwani kitendo hicho cha utekaji kimezua maswali mengi.
Akizungumzia kupatikana kwa watoto hao Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema baada ya mahojiano na mtuhumiwa alikiri kuwateka na kuwauwa watoto hao.
Mkumbo amesema mtuhumiwa alikamatwa mkoani Geita alikokimbilia baada ya kuwateka watoto wanne ambapo wawili kati yao walipatikana wakiwa hai.

SECHELELA KONGOLA
SEPTEMBA 07, 2017