Natumia nafasi yangu - Ndugai
Spika wa Bunge, Job Ndugai amefunguka na kusema kuwa yeye hana tatizo lolote na Mbunge Zitto Kabwe, Saed Kubenea na Godless Lema ila amedai yeye ni binadamu hivyo mtu anapomnyanyasa na kumdhalilisha hutumia mamlaka aliyonayo kufanya maamuzi.
Spika wa Bunge, Job Ndugai. |
Ndugai amesema kuwa yeye kama kiongozi wa Bunge anamamlaka na madaraka makubwa kuliko hata yaliyoandikwa na kusisitiza kuwa anao uwezo wa kumsimamisha Mbunge asiongee chochote bungeni mbaka muda wa mbunge huyo utakapokwisha.
"Siyo kila kitu huandikwa katika mahusiano ya kikazi lakini kiongozi wako wa kazi ana mamlaka na madaraka makubwa kuliko hata yaliyoandikwa si kila jambo lazima liwe ni kanuni, narudi tena nimesikia watu wakibisha bisha ninao uwezo kama spika, zipo kanuni zinamruhusu Spika wa Bunge kwa kadri anavyoona inafaa kwa busara yake namna gani aongoze bunge, huwezi kuwa unatukana bunge unamtukana huyo spika halafu huyo huyo Spika anakupa nafasi uzungumze kwa sababu yeye ni malaika? Mimi ni binadamu mwenye damu na nyama kama wengine" alisema Ndugai
Spika wa Bunge aliendelea kutoa ufafanuzi juu ya baadhi ya wabunge ambao wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kupotosha umma au kumzungumza mambo ya bunge kwa njia isiyo na staa kupitia mitandao hiyo ya kijamii na kumdhalilisha yeye na kusema yeye pia atatumia mamlaka yake kuona anafanya nini juu ya wabunge hao.
"Kwa jinsi unavyoninyanyasa na kunidhalilisha mbele ya watu na mimi nitatumia madaraka yangu na mamlaka niliyonayo niliyopewa na nchi na Mungu kuona nini nifanye katika mamlaka niliyonayo" alisisitiza Ndugai
Spika wa Bunge Job Ndugai alisema kuwa ana uwezo wa kumzuia mbunge Zitto Kabwe asizungumze chochote ndani ya bunge kwa kipindi chote cha ubunge
Post a Comment