Ajali yaua mmoja na kujeruhi
Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina moja la William amefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa vibaya baada ya lori walilokuwa wakisafiria kupasuka gurudumu la mbele upande wa kushoto na kuacha njia eneo la gogoni Kibamba Manispaa ya Ubungo.
Ispector wa Polisi wa kituo cha Kimara, Seni Magembe amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema imetokea majira ya saa 3 asubuhi huku majeruhi wa ajali hiyo akiwepo dereva wa lori hilo Shabani Ramadhani (29) amelazwa katika hospitali ya Tumbi pamoja na mwili mwili wa marehemu Wiliam ambaye alikuwa utingo wa lori lenye namba za usajili T. 955 ACP aina ya Volvo likiwa na tela lake lenye namba T 724 AAN umehifadhiwa katika hospitali hiyo hiyo ya Tumbi.
Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo Abuu Ramadhani mkazi wa Gogoni amesema walisikia kishindo kikubwa majira ya saa 3 asubuhi na walipofika eneo hilo maarufu kama Gogoni kwa bi Mtumwa walikuta gari hilo likiwa tayari limepinduka.
Ajali hiyo imetokea wakati jeshi la polisi mkoani Pwani , kitengo cha Usalama barabarani likiendelea na operesheni maalumu ya ukaguzi wa makosa mbalimbali ya barabarani kwa madereva wa malori sambamba na kuwapima kiwango cha ulevi .
Post a Comment