Usiyoyajua kuhusu msimu mpya wa UEFA
Msimu mpya wa 2017/18 ligi ya mabingwa Ulaya unafunguliwa rasmi leo kwa jumla ya mechi nane kupigwa kutoka kwenye makundi manne.
Rekodi mbalimbali zinatarajiwa kuwekwa na zingine kuvunjwa ikiwemo ile ya mchezaji aliyecheza misimu mingi zaidi ambaye ni Iker Cassilas, golikipa wa zamani wa Real Madrid ambaye hivi sasa anakipiga na klabu ya FC Porto ya Ureno atakuwa anacheza msimu wake wa 19 watakapokabiliana na Besikitas kesho.
Cristiano Ronaldo anashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika hatua ya makundi ndani ya msimu mmoja akiwa na mabao 11. Mpinzani wake Lionel Messi anashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi kwenye hatua ya makundi akiwa amefunga mabao 57 katika misimu yake yote aliyocheza UEFA.
Klabu za RB Leizpzig na Qarabag ndio timu mpya kwenye michuano hiyo na zitacheza kwa mara ya kwanza tangu zianzishwe. Baada ya misimu 15 kupita klabu ya Fayenood kutoka Uholanzi inarejea kwenye michuano hiyo ikiikaribisha Manchester City ya Engalnd.
Mchezo utakaotazamwa zaidi hii leo ni kumbukumbu ya fainali ya UEFA mwaka 2015 kati ya Barcelona na Juventus utakaopigwa Camp Nou Hispania.
Ratiba Kamili
Sep 12, 2017
Kundi A
Benifika vs CSKA Moscow
Manchester United vs Basel
Kundi B
Bayern Munchen vs Anderlecht
Celtic Vs Paris Saint Germain
Kundi C
Chelsea vs Qarabag FK
Roma vs Atletico Madrid
Kundi D
Barcelona Vs Juventus
Olympiacos vs Sporting CP
Post a Comment