WAZEE 2376 WAPATIWA VITAMBULISHO KIGAMBONI.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amekabidhi vitambulisho 2376 kwa wazee kwaajiri ya matibabu.


Akikabidhi vitambulisho hivyo ambavyo vitawasaidia wazee kwenye huduma za matibabu bila kutoa malipo yoyote,Waziri mwalimu amesema kuwa madaktari wawajali wazee kwani nao ni wazee watarajiwa. Wazee hawa wakija wahudumiwe na si kuwadharau na kuwaweka kwenye foleni kwa muda mrefu.
Pia Mhe.Mwalimu ameupongeza uongozi wa manispaa ya kigamboni kwa maendeleo makubwa walioyafanya kwa kipindi cha mwaka mmoja.
"Nawaakikishia katika jiji hili la kigamboni mmekuwa wakwanza kutekeleza jambo hili tena kwa kiwango kikubwa".Alisema Mhe.Mwalimu.

Naye mzee Ismail Hamis Mndenga(63) alishukuru sana kukabidhiwa kitambulisho hicho na kusema kuwa anaona kama tiba maana huku nyuma alikuwa anapata shida ya kupata matibabu kutokana na mlolongo uliokuwepo.


Pia Mhe.Waziri mwalimu,Aliwapongeza watumishi kwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi na kujituma.

Vile vile kufuatia tatizo la ukosefu wa dawa na ucheleweshwaji wa upatikanaji wa dawa,Mhe.Mwalimu alisema kuwa kwa sasa bajeti ya dawa imeongezeka katika kila hospitali mfano,Kabla ya vijibweni ilipata milioni 22 lakini kwa sasa bajeti iliyopangwa ni shilingi milioni 57.
Halimashauri ya manispaa ya kigamboni inakadiriwa kuwa na wazee 7000 wanaotajika kunufaika na huduma hii.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA TEHAMA 

HALIMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI.