VENEZUELA YAIBUKA MGOMO ULISABABISHA GHASIA KALI.
Mamilioni ya Wavenezuela wameitikia
wito wa Upinzani wa kubakia nyumbani, katika mgomo wa kwanza wa saa 24
kufanyika nchini humo kwa zaidi ya muongo mmoja.
Hatua hiyo ni kupinga mipango ya serikali ya kuandika tena katiba mpya.
Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi katika miji kadhaa, walipopambana na waandamanaji.
Katika ghasia hizo waandamanaji watatu waliuawa.
Hata hivyo, katika maeneo yanayounga mkono serikali ya nchi hiyo mjini Caracas, maisha yaliendelea kama kawaida.
Katika
hotuba yake kupitia televisheni, Rais Nicolas Maduro amesema mamia ya
wafanyabiashara waliendelea na shughuli zao kama kawaida na kwamba
viongozi wa mgomo huo watakamatwa.
Lakini upinzani nao umedai kuwa
Rais Maduro anajaribu kujiimarisha madarakani kwa kubadili katiba,
hali ambayo itabadili hali ya sasa ya upinzani kudhibiti bunge.
Na katika Umoja wa Mataifa mwanadiplomasia wa Venezuela amejiuzulu katika kupinga hatua zinazochukuliwa na serikali yake.
Post a Comment