MANCHESTER UNITED YAILAZA MANCHESTER CITY DEBI YA UGENINI.
![]() |
Romelu Lukaku na Marcus Rashford wakisherehekea ushindi wa mabao yao |
Manchester United
imejipatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wapinzani wao wa jadi
Manchester City katika debi ya kwanza ugenini huku ziara za 2017
zinazofadhiliwa na Aon zikiendelea kuipatia ushindi the red Devils.
Romelu Lukaku na Marcus Rashford waliisaidia United katika mabao yote mawili yaliofungwa katika kipindi cha kwanza.
Kikosi
hicho cha Jose Mourinho kilianza kwa mashambulizi huku Anders Herrera
akianzisha juhudi hizo mapema, huku mashambulio mengine yakitoka nje ya
eneo la hatari ,United wakimjaribu kipa mpya wa City Ederson.
David
De Gea alilazimika kuwa macho katika upande mwengine huku Raheem
Sterling akishambulia mara mbili , kabla ya Chris Smalling kuzuia
mashambulizi mawili yaliofanywa na Patrick Roberts na Sterling.
United
hatahivyo ilifanikiwa dakika nane kabla ya kukamilika kwa kipindi cha
kwanza baada ya Lukaku kupata pasi muruwa kutoka kwa Paul Pogba na
kucheka na wavu.
Dakika mbili baadaye Marcus Rashford aliifungia United bao la pili akifunga baada ya kazi nzuri kutoka kwa Henrikh Mkhitaryan.
Post a Comment