NDEGE ZA KUTOKA SAUDI ARABIA HADI MAREKANI ZAONDOLEWA MARUFUKU YA LAPTOPS


Marufuku ya laptopu ndani ya ndege zinazofanya safari ya moja kwa moja kutoka nchini Saudi Arabia hadi Marekani imeondolewa, kwa mujibu wa shirika la ndege la Saudi Arabian.
Linasema kuwa viwanja vya ndege ambavyo ndege zinazoelekea Marekani hutumia, vimeruhusiwa na idara ya ulinzi ya Marekani.
Uwanja wa King Khalid mjini Riyadh ndio wa mwisho kati ya viwanja kumi vilivyoondolewa marufuku hiyo.
Mwezi Machi Marekani ilipiga marufuku laptopu na vifaa vingine vikubwa vya elektroniki kutoka nchi nane za kiislamu.

Mashirika ya Kuwait Airways na Royal Jordanian yamekuwa ya hivi punde kuruhusu abiria kubebea laptopu ndani ya ndee zinazoelekea Marekani.
Mashirika hayo mawili yalisema yameshirikiana na maafisa wa Marekani kuimarisha usalama kwa ndege zinazotoka nchini Kuwait na Jordan.
Marekani ilitangaza marufuku hiyo mwezi Machi kwa safari za moja kwa moja kutoka nchi nane za kiislamu kutokana na hofu kuwa mabomu yangebebwa ndani ya vifaa hivyo.
Mashirika ya ndege ya Etihad, Turkish Airlines, Emirates and Qatar yaliondolewa marufuku hiyo wiki iliyopita.
Shirika la Royal Jordanian ambalo hufanya safari katika miji mitatu ya Marekani kutoka Amman, mji mkuu wa Jordan, liliondoa marufuku hiyo baada ya hatua mpya za kiusalama zilizochukuliwa kwenye ndege zinazoelekea nchini Marekjni.
Shirika linalomikiw na serikali la Kuwait Airlines ambalo hufanya safari zake kutoka Kuwait kuenda mjini New York likipitia Ireland lilisema kuwa marufuku hiyo ilitolewa baada ya maafisa wa Mareknian kukagua usalama kwenye safari zake

 Viwanja wa King Abdulaziz mjini Jeddah na King Khalid mjini Riyadh vyote vimekaguliwa na kuruhusiwa laptopu kuingia viwanjani humo.
Viwanja hivyo viwili vinatumiwa na ndge zinazosafiri moja kwa moja kutoka Saudi Arabia kwende Marekani.
Shirika la ndege la Saudi Arabian ambalo pia linajulikana kama Saudia ndilo pekee ambalo hufanya safari za moja kwa moja kuenda Marekani.