UCHIMBAJI NA UCHOTAJI MCHANGA KIHOLELA WASITISHWA BUNJU
Eneo
la mto Nyakasangwe lililopo kaika kata ya Bunju linavyoonekana
kuharibika vibaya kutokana na uchimbaji wa mchanga , na kupelekea makazi
ya wananchi kuwa hatarini.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina
akizungumza na vyombo vya habari baada ya kukamilika kwa zoezi la
kukagua mto Nyakasangwe, uliopo katika kata ya Bunju ulioharibiwa vibaya
na uchimbaji wa mchanga.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina
akimsikiliza Mwandishi wa Habari wa kituo cha Radio cha Efm
kinachopatikana katika masafa ya 93.7 katika jiji la Dar es Saalam
alipokuwa akimuuliza maswali kuhusu uchafuuzi wa mazingira utokanao na
uchimbaji wa mchanga katika eneo la Boko.
……………………………………………………………….
NA; EVELYN MKOKOI
NAIBU
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina
,amesitisha uchimbaji na uchotaji wa mchanga kiholela katika maeneo
yasiyo rasmi.
Pia
ametoa siku 30 kwa Halmashauri za Manispaa za Jiji la Dar es Salaam
kubaini na kutenga maeneo ya uchimbaji ya mchanga ambayo yapo ndani ya
manispaa zao yatakayo ruhusiwa kwa zoezi hilo kisheria.
Akitoa
agizo hilo Dar es Salaan leo,wakati wa ziara ya kutembelea Mto
Nyakasangwe uliopo maeneo ya Boko Kata ya Bunju alisema kama kuna maeneo
ambayo wananchi wanaweza kufika Kwa urahisi, manispaa zinapaswa
kuyatembelea maeneo hayo na kuyabaini kama kunauwezekano wakuchimba
mchanga.
Alisema
ndani ya mwezi mmoja manispaa hizo zinatakiwa kuandaa utaratibu mfupi
wa kutenga maeneo hayo ikiwemo utoaji wa vibali kutoka Wizara ya Nishati
na Madini,Halmashauri pamoja na Nemc.
“Halmashauri
zote zilizo na eneo ambalo linaweza kuruhusiwa kuchota mchanga
hakikisheni mnatembelea maeneo hayo na kufata taratibu zote za utoaji wa
vibali ambapo maeneo mengine yawe ya uchotaji wa mchanga,”alisisitiza
Mpina
Alisema
watafanya Operasheni ya usiku na mchana kuhakikisha watu
watakaoendelea kuchimba mchanga na kuchota mchanga sehemu ambazo
haziruhusiwi watachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kutozwa faini
zilizopo kisheria na kufikishwa mahakamani.
Kwa
upande wake diwani wa kata ya Bunju Bw. Kateni Nassor Msangi
alimshukuru Mpina kwa kufanya ziara katika eneo hilo na kuiomba serikali
kufanya utaratibu wa kujengea mawe katika kuta za kingo yam to huo
ambao umeharibika vibaya, ili kuweza kunusuru mazingira ya mto huo
kuharibika pamoja na kunusuru makazi yao.
Post a Comment