TSN na MIMOSA wasaini mkataba wenyetija hizi
TSN
Group Tanzania, katika kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wateja wake
hapa nchini, imeingia mkataba na MIMOSA CONCIERGE inayotoa MIMOSA Black
Card ambayo ni kadi maalum kwa wateja wanaofika kupatiwa huduma kupitia
kadi hizo.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa kusaini mkataba huo na kampuni hiyo
jijini Dar es Salaam, leo Meneja Masoko wa TSN alisema, Jahu M. Kessy
amesema TSN imelenga kuongeza tija katika kutoa huduma zake.
“Tunarahisisha
na kuboresha huduma zetu kuwa bora na za kisasa. Pengine huduma hii
itapanua wigo wa wateja wetu watumiao Black Cards kwa Dar es salaam
lakini kwa Mwanza TSN Hypermarket inakuwa kampuni ya kwanza kupokea na
kukubali malipo kupitia Black card ya Mimosa. Hatua ambayo ni kubwa
kuchukuliwa na TSN katika kuwajali wateja wake.”
“Sasa
ukifanya malipo kupitia kadi ya Mimosa kwenye supermarket zetu na
Petrol station unajiweka katika nafasi ya kushinda punguzo la zaidi ya
asilimia 5 pamoja na kuponi ya zawadi wa kwateja watakao tumia kiasi cha
shillingi laki moja kwa manunuzi ya mara moja,” alisema Jahu.
Akieleza
zaidi juu ya huduma na faida wazipatazo wateja watumiayo kadi hizo,
Mkurugenzi Msiaidizi wa MIMOSA, Leonce Mongi alisema kupitia kadi hii
Mteja wa TSN hatapata tu punguzo la bei kutoka TSN pekee lakini pia
atapata offer mbalimbali zitokanazo na kadi hiyo kupitia discount
partners wengine ambao ni zaidi ya watoa huduma 71 Nchi Nzima.
Jahu
alisema TSN inajiimarisha katika kutoa huduma zake kwa wateja,
kuwasikiliza na kuwasaidia, hivyo basi kuona umuhimu wa kuwapatia wateja
wake wenye MIMISA black card nafasi ya kufanya malipo yao kwa uhuru na
furaha.
Alisema,”hatua
hii inafuatia hatua nyinginezo nyingi tulizochukua kuhakikisha wateja
wa TSN wanafurahia huduma zetu, ikiwemo malipo kutupitia miamala ya
simu, bank cheques, malipo ya dola na sasa pia kupitia Mimosa Black
Card.
Leonce
alisema kupitia kadi hii TSN itakuwa ikipokea malipo na kuongezaa tija
kwa mteja, lengo ni kuhakikisha mteja mwenye kadi ya Mimosa hashindwi
kufanya malipo yake akiwepo katika vionga vyao, na pia kufurahia ofa na
punguzo mbalimbali zipatikanazo na mtangamano huu.
“Teknolojia
imeendelea kuwa kitovu cha maendeleo ya jamii yetu kwa kurahisisha na
kuongeza ufanisi katika utendaji kazi. Kukua kwa teknolojia katika
nyanja mbalimbali za kiuchumi kisiasa na kijamii kumeendelea kuleta
matokeo chanya siku hadi siku. Sambamba na kurahisishwa kwa utendaji
kazi lakini pia upokeaji wa huduma mbalimbali za kijamii kwa wananchi wa
kawaida kumerahisishwa.” Alisema Jahu.
Katika
kutambua fursa hiyo, TSN itaendelea kujidhatiti katika kuhakikisha kuwa
huduma kwa wananchi zinaenda sambamba na mabadiliko hayo ya teknolojia.
Leonce
aliipongeza TSN kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inaweka
urahisi kwa wateja wake na hiyo imekuwa ni chachu kubwa katika
kurahisisha utoaji huduma kwa wateja wao.
Post a Comment