ISRAEL YAWEKA KAMERA ZA ULINZI ENEO TAKATIFU MJINI YERUSALEM
Israil imeweka kamera pahala wa kuingia katika uwa wa msikiti wa al-Aqsa katika mji mkongwe wa Jeruslem.
Hayo
yanatokea wakati wa mvutano mkubwa kuhusu hatua za usalama kwenye eneo
hilo, ambalo waislamu wanali-ita Haram al-Sharif na wayahudi wanaita
Temple Mount.
Waumini wa Palestina wamepinga vikali Israil kuweka
mitambo ya kun'gamua kama mtu amebeba kitu cha chuma, baada ya askari
polisi wawili wa Israil kuuwawa.
- Rais wa Palestina akata mawasiliano na Israel
- Israel yafungua eneo takatifu Jerusalem
- Polisi wawili wa Israel wauawa Jerusalem
- Waziri mkuu wa zamani wa Israel aliye gerezani kuachiliwa
Wapalestina watatu waliuawa wakati wa ghasia na vikosi vya
Israel
siku ya Ijumaa, wakati maelfu waliandamana mashariki mwa
Jerusalem na eneo la linalomilikiwa na Israel la Ukingo wa Magharibi.
Baadaye
raia watatu wa Israel wakauawa kwa kuchomwa visu katika makao ya
walowezi wa kiyahudi karibu na Ramallah na mshambuliaji mpalestina
ambaye aliingia nyumbani kwao.
Post a Comment