RAIS MAGUFULI AAMWAGIA SIFA MBUNGE WA KALIUA,(CUF) MAGNALENA SAKAYA.


Rais John Magufuli amemmwagia sifa mbunge wa Kaliua, (CUF) Magdalena Sakaya na kusema kuwa mwili na tabia yake ni za CUF lakini roho na damu yake ni ya CCM.

Ameyasema hayo leo Jumapili, Julai 23 wakati wa ziara yake mkoani Tabora na kuwataka wabunge wa CCM kumpa ushirikiano anapofanya shughuli za maendeleo.

“Inawezakana hata siku zijazo akahamia CCM, damu yake na roho yake ni CCM ingawa mwili na maneno na tabia zake ni CUF,” amesema.

Amesema ni mara kumi uwe na CUF, Chadema au NCCR anayefanya mambo ya CCM kuliko uwe na CCM anayefanya mambo ya vyama vingine.

“Hasara yake ni kubwa mno, mnafikiri ni mwenzenu wakati siyo mwenzenu, nani hayajui haya hata wakati wa kampeni yalitokea unafikiri siyajui,” amesema.

Amewataka wabunge wa CCM kumpa ushirikiano Sakaya na kuwataka wasimbague kama asivyowabagua