BUNGE LA CONGRESS LAAFIKIA MAKUBALIANO YA KUIWEKEA URUSI VIKWAZO VIPYA
Image caption
Viongozi kutoka
vyama vyote katika bunge la Marekani wamekubaliana kuhusu sheria ambayo
inaruhusu vikwazo vipya kuiadhibu Urusi kwa kuingilia uchaguzi wa
Marekani.
Sheria hiyo pia itapunguza uwezo wa Rais Donald Trump wa kuiondolea Urusi vikwazo.
Kipindi cha bwana Trump ofisini kimekumbwa na madai kuwa Urusi ilisaidia kushawishi uchaguzi wa mwaka uliopita.
Urusi
inakana kutenda lolote baya la uchunguzi kadha ambao umefanywa na
Marekania unatathmini ikiwa yeyote katika kampeni ya Trump alishirikiana
na maafisa wa Urusi.
Waandishi wa habari wanasema kuwa
makubaliano hayo ya Congress, yanaonyesha msimamo uliopo dhidi ya Urusi
bila kujali maoni ya Trump.
- Urusi kuwatimua wanadiplomasia 30 wa Marekani
- Maafisa wa Marekani na Urusi kukutana
- Urusi yashutumu shambulio la Marekani dhidi ya Syria
- Trump na Putin wajadiliana kuhusu udukuzi wa uchaguzi wa Marekani
Rais anaweza kuukataa mswada huo, lakini kwa kufanya hivyo inaweza kushukiwa kuwa anaiunga mkono Urusi.
Kwa upande mwingine ikiwa atautia sahihi itakuwa ni kuidhinisha sheria ambayo utawala wake unaipinga.
Mswada huo poia unaruhusu vikwazo zaidi dhidi ya Korea Kaskazini na Iran.
Sheria
hiyo itaruhusu vikwazo vipya dhidi ya Urusi kwa kulimega eneo la Crimea
mwaka 2014 na madai ya kuingilia uchaguzi wa Marekani.
Post a Comment