Hospitali Teule ya Mkoa wa Geita yapongezwa
KISIGINO HABARI
Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na watoto Ummy Mwalimu akiongea na watoa huduma
kwenye hospitali teule ya rufaa ya Mkoa wa Geita wakati alipofanya ziara
ya kikazi katika hospitali hiyo ambapo aliridhishwa na huduma
zitolewazo na hospitali hiyo na kuwapongeza kwa kuanzisha kitengo cha
ubora za huduma za faya ambacho kinasaidia kuimarisha afya ya wagonjwa
ikiwemo mama na mtoto pamoja na lishe.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo Meja
Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga na nyuma ya Waziri ni Katibu Tawala wa
Wilaya ya Geita Thomas Dimme.
Waziri Ummy akimjulia hali akina
mama waliojifungua katika wodi ya Wazazi.Akina mama hao walikiri
kuhudumiwa vizuri na watoa huduma hiyo pia hawajatozwa fedha yeyote kama
sera ya afya inayosema kila mama mjamzito matibabu ni bure
Mhudumu wa afya pekee wa kike
katika chumba cha kuhifadhi maiti Bi.Angela Milinga(mwenye koti jeupe)
ambaye anafanya kazi katika hospitali hiyo akimshukuru Waziri Ummy kwa
kufika katika kitengo chake na kujionea jinsi wanavyofanya kazi .
Mhudumu wa chumba cha kuhifadhia
maiti Bi. Anjela akieleza jinsi anavyofanya kazi kwa Mhe. Waziri (hayupo
pichani) mara baada ya kutembelewa na ugeni huo.
Watumishi wa hospitali hiyo
wakimsikiliza Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto(hayupo pichani) wakati wa mkutano wa ndani mara baada ya
kutembelea sehemu mbalimbali za kutolea huduma za hospitali hiyo
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita,Dkt.
Joseph Kisala akisoma taarifa ya hospitali hiyo,Kulia ni Mbunge wa
Jimbo la Geita mjini Mhe.Costantine Kanyasu na Kushoto ni Mganga
Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Brian Mawalla
Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo
Dkt. Brian Mawalla akimfafanulia jambo Waziri wa afya(hayupo pichani)
wakati wa mkutano na watumishi wa hospitali hiyo
Picha ya Pamoja ya Waziri Ummy
Mwalimu, Viongozi wa Mkoa,Wilaya na watumishi wa hospitali hiyo mara
baada ya kumaliza mkutano wa ndani.Katika kikao hicho Waziri aliwataka
wafanyakazi ambao hawataki kubadilika na kuwajibika wakati wa
kuwahudumia wagonjwa wapishe kwani hivi sasa kuna wahitimu wengi
wanahitaji ajira Serikalini hususan kada ya afya(Picha zote na Wizara ya Afya)
Post a Comment