Rais atangaza mpango wa kutengeneza fedha mpya

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ametangaza mpango wa kutengeneza fedha mpya ya nchi hiyo katika kujaribu kuunusuru uchumi wa nchi hiyo.
Amesema fedha hiyo iitwayo Petro itaimarishwa na utajiri wa Venezuela utokanao na mafuta, gesi, pamoja na dhahabu.
Uchumi wa Venezuela umedorora mno kutokana na kushuka kwa mapato ya mafuta pamoja na kuporomoka kwa thamani ya fedha yake ya sasa ya bolivar.