Kigwangalla aibua mengine bandarini

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Kigwangalla, ameagiza Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii atangaze kujitokeza kwa wamiliki wa magogo 938 yaliyokaa bandarini kwa zaidi ya miaka 10. Kama wamiliki wasipojitokeza, magogo hayo yatakuwa mali ya Serikal
Kigwangalla ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Bandari ya Dar es salaam hapo kufuatia uwepo wa taarifa za uvunaji holela wa magogo nchini, ambapo kuna taarifa kuwa kuna wafanyabiashara wa kigeni wanagawa vifaa vya kuvunia bure kwa ahadi ya kuuziwa mzigo na wahusika.
Aidha taarifa zingine zilizosababisha ziara hiyo kufanyika ni kuwepo  habari kwamba kuna baadhi ya watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wanatoa vibali na kugonga nembo kinyume cha taratibu za kisheria. Hali inayotishia usalama wa raslimali adimu ya misitu ya asili.
Mbali na hayo Dkt Kigwangalla ametoa siku 30 kwa wamiliki wa makontena 55 yanayodaiwa kuingizwa nchini kutoka Zambia kujitokeza na kuwasilisha nyaraka zao zenye kuthibitisha kama kweli yalivunwa nchini Zambia na yalivunwa wapi na kwa vibali gani vya nchi hiyo, Pia kufuatilia nyaraka za kuingiza ndani ya Tanzania. 
Ameagiza kitengo cha kuzuia ujangili kifuatilie kubaini uhalisia na uhalali wa taarifa hizo vinginevyo yatakuwa mali ya Serikali.