CHADEMA wazungumza Mnyika kujivua uanachama

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimekanusha habari inayoenea kuhusu Mbunge wa Kibamba, John Mnyika kujivua uanachama kuwa hazina ukweli wowote na zinapaswa kupuuzwa
Chadema wametua kanusho hilo kupitia mtandao wa Twittter kwenye ukurasa wa chama hicho na kusma kwamba wanaosambaza habari za Mnyika kujivua ni wale walioishiwa hoja na majibu juu ya maisha ya watanzania.
"Kuna taarifa zinasambazwa mitandaoni ya kuwa Mhe. John Mnyika, Mbunge wa Kibamba amejivua uanachama wa CHADEMA. Taarifa hizo ni za uongo na hazina ukweli wowote, ni za kupuuzwa, wanaozisambaza ni wale walioishiwa hoja na majibu juu ya hali ya maisha ya Watanzania".