Watu nane wauawa kigaidi

Watu 8 wameuawa na zaidi ya 12 kujeruhiwa baada ya mwanaume mmoja wa miaka (29) kuwashambulia na gari waendesha baiskeli na watembea kwa miguu, nchini Marekani.
Kamishna wa polisi wa jiji la New York, James O'Neill, amemuelezea mtu aliyetekeleza tukio hilo kuwa ni kijana wa miaka 29 aliyekuwa anaendesha gari ndogo la kubebea mizigo alilokuwa amelikodi.
Amesema gari hilo liliwagonga watembea kwa miguu na wapanda baiskeli kabla ya kugongana na basi la shule.
Kwa upande wake bwana O'Neill, amesema kuwa dereva wa gari hilo alitoka ndani ya gari lake na kuanza kuandaa silaha mbili kwa ajili ya shambulizi na kufafanua  kabla ya kutekeleza azma yake  polisi walimuwahi na kumpiga risasi zilizomjeruhii.
Polisi mjini humo wametoa tamko kwamba wanalichukulia tukio hilo kama shambulizi la kigaidi na mtuhumiwa wa tukio hilo amechukuliwa na polisi kwa mahojiano zaidi ambao walithibitisha taarifa hizo katika kituo cha Lower Manhattan.
Vyombo vya habari nchini Marekani vimenukuu taarifa za polisi kuwa kijana huyo aliamua kuendesha gari hilo katika njia ya waendesha baiskeli iliyoko karibu na Mto Hudson eneo la Lower Manhattan ya chini kabla ya kupigwa risasi na maafisa wa polisi ili kuzuia shambulio alilolipanga.